Home Vipindi Matukio ya Taifa: Takriban waathiriwa 10 wa mlipuko wa gesi huenda wakakabiliwa...

Matukio ya Taifa: Takriban waathiriwa 10 wa mlipuko wa gesi huenda wakakabiliwa na matatizo ya figo

0

Takriban waathiriwa 10 ambao waliathiriwa na mlipuko wa mtungi wa gesi huko Embakasi Alhamisi iliyopita huenda wakakabiliwa na matatizo ya figo katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Kulingana na takwimu za Taasisi ya Kitaifa ya Afya, kati ya wahathiriwa 100 waliolazwa katika hospitali mbalimbali, zaidi ya 20% yao wameungua, ambayo inaweza kuwa kichocheo cha kushindwa kwa figo.