Serikali kuu imeanza zoezi la kukusanya data kuhusu athari za mvua kubwa inayoendelea kuathiri maeneo mengi nchini.
Naibu rais Rigathi Gachagua amesema ripoti hiyo itawekwa wazi baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo, ambayo habari kuhusu waliosombwa na mafuriko, mifugo na mimea iliyoathirika itajumuishwa kwenye ripoti hiyo.