Home Habari Kuu Matozo mapya ya SHIF kuanza mwezi Machi mwaka huu

Matozo mapya ya SHIF kuanza mwezi Machi mwaka huu

0
Waziri wa afya Susan Nakhumicha.

Waziri wa afya Susan Nakhumicha, amefichua kuwa bima mpya ya afya SHIF  itaanza kutekelezwa mwezi Machi mwaka huu.

Waziri Nakhumicha alifichua  hayo Alhamisi akiongeza kuwa wakaribia kukamilisha vipengee na sheria zinazoambatana na bima  hiyo,kabla ya kuanza kutekelezwa  rasmi.

Nakhumicha aliongeza kuwa bima hiyo  itasimamia kila Mkenya huku wanaotaka huduma maaluma za matibabu, wakihitajika kulipia ada za zaidi kando.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Waziri alisema kuwa matozo mapya  ya bima hiyo, yataanza kukatwa kwenye mishahara ya wafanyikazi kuanzia mwezi  Machi .

 

Website | + posts