Home Habari Kuu Matokeo ya mitihani ya KCPE na KPSEA kutangazwa Alhamisi

Matokeo ya mitihani ya KCPE na KPSEA kutangazwa Alhamisi

Hafla hiyo itaandaliwa katika afisi za baraza la kitaifa la mitihani hapa nchini KNEC, katika mtaa wa South C Jijini Nairobi.

0

Matokeo ya mwaka 2023 ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane, KCPE na tathmini ya darasa la sita, KPSEA yanataraajiwa kutangazwa leo Alhamisi, Novemba, 23, 2023.

Wizara ya Elimu imesema zoezi hilo litaongozwa na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, kuanzia saa mbili asubuhi.

Hafla hiyo itaandaliwa katika afisi za Baraza la Kitaifa la Mitihani Nchini KNEC, katika mtaa wa South C jijini Nairobi.

Katibu wa elimu ya msingi Dkt. Belio Kipsang na afisa mkuu mtendaji wa KNEC Dkt. David Njengere,ni miongoni mwa wale watakaohudhuria hafla hiyo.

Takriban wanafunzi milioni 1.4 walifanya mtihani wa KCPE huku wanafunzi milioni 1.2 wakifanya  KPSEA.

Wanafunzi wa mwaka huu wa darasa la nane, ndio walikuwa wa mwisho kufanya mtihani wa KCPE, huku wakitamatisha mfumo wa elimu wa 8-4-4, baada ya kuanzishwa kwa mfumo mpya wa elimu wa CBC, ambao unatekelezwa kwa sasa.