Home Kimataifa Matokeo ya KCPE yaliyotumwa kupitia SMS kufanyiwa ukaguzi, asema Machogu

Matokeo ya KCPE yaliyotumwa kupitia SMS kufanyiwa ukaguzi, asema Machogu

0
kra

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema matokeo ya wanafunzi wa KCPE mwaka huu yaliyopokelewa kupitia arafa yatafanyiwa ukaguzi wa kina kubaini chanzo cha dosari.

Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya elimu katika bunge la seneeti jana Alhamisi, Machogu alisema tayari ameiandikia Wizara Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali yake Eliud Owalo kuomba utathmini wa kina kuhusu matokeo hayo yaliyotumwa na kampuni iliyopewa zabuni.

kra

Machogu aliahidi kuwa uchunguzi huo utakamilika baada ya siku 14 na ripoti kamili kutolewa.

Matokeo ya mwaka huu kwa darasa la mwisho la mfumo wa 8-4-4, yalikumbwa na dosari kadhaa huku wadau wa elimu wakihoji uhalali wake.

Website | + posts