Home Michezo Mateiko awaongoza Wakenya kutamalaki RAK Half Marathon

Mateiko awaongoza Wakenya kutamalaki RAK Half Marathon

0

Daniel Mateiko Kibet amewaongoza Wakenya kutwaa nafasi zote za kwanza tatu katika makala ya mwaka 2024 ya mbio za Nusu marathon za Rasl Al Khaimah, maarufu kama RAK mapema Jumamosi katika Milki za Kiarabau.

Mateiko ambaye alikuwa mmoja wa wapiga kasi wa marehemu Kelvin Kiptum akivunja rekodi ya dunia mwaka jana katika mbio za Chicago,ameziparakasa mbio hizo kwa dakika 58 na sekunde 45,akifuatwa na John Korir kwa dakika 58 na sekunde 50, huku Isaia Lasoi akimaliza wa tatu sekunde 5 baadaye.

Margaret Chelimo,Evaline Chirchir ,Catherine Amangole na Peres Jepchirchir walimaliza katika nafasi za 4,5,6 na 7 katika mbio za wanawake .

Tsigie Gebreselama na Ababel Yeshaneh wote kutoka Ethiopia wamenyakua nafasi za kwanza pili kwa muda wa saa 1 dakika 5 na sekunde 14 na saa 1 dakika 5 na sekunde 44 mtawalia ,huku Jackline Juma Kasilu wa Tanzania akiridhia nafasi ya tatu.

Website | + posts