Home Michezo Matayarisho ya michezo ya Wabunge Afrika Mashariki yanoga

Matayarisho ya michezo ya Wabunge Afrika Mashariki yanoga

0
kra

Matayarisho kwa makala ya 14 ya michezo baina ya Wabunge wa Afrika Mashariki yameshika kasi, huku michezo hiyo ikitarajiwa  kuandaliwa Disemba mwaka huu.

Kamati ya pamoja ya maandalizi ikiongozwa na Mbunge wa Afrika Mashariki Kanini Kega, ilizuru viwanja vitakavyoandaa mashindano hayo kati ya Disemba 6 na 18.

kra

Viwanja vitakavyoandaa michezo hiyo ni pamoja na KPA Mbaraki Sports Club, Aga Khan Academy, Mombasa Sports Club, Nyali Golf, Shanzu Teachers Training College, Sheikh Zayed, KPA Highlife, na Mombasa ASK Showground.

Kulingana na Kega mataifa manane wanachama wa EAC ikiwemo Somalia,yatashiriki katika fani za riadha ,soka,mpira wa kikapu ,uvutaji jugwe ,vishale kwa walemavu na gofu.

Zaidi ya Wabunge 1500 na wafanyikazi wa mabunge ya Afrika Mashariki watashiriki mashindano hayo, yanayohimiza mtagusano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kega pia ametoa changamoto kwa serikali ya kitaifa na zile za kaunti kuwekeza kwenye muundombinu wa viwanja kukomesha hali ilivyo kwa sasa, ambapo viwanja vyote vitakavyoandaa mashindano ya mwaka huu ni vile vya kibinafsi.

Website | + posts