Home Michezo Matarishi Posta warejelea tambo za ushindi baada ya ukame wa mechi tatu

Matarishi Posta warejelea tambo za ushindi baada ya ukame wa mechi tatu

0
kra

Posta Rangers wamesajili ushindi wa kwanza tangu Novemba 25, baada ya kuwazabua Ulinzi Stars mabao mawili kwa bila uwanjani Ulinzi Complex, katika mojawapo ya mechi nne za ligi kuu zilizosakatwa Alhamisi.

Rangers walipata magoli yao kupitia kwa Brian Otieno na Patrick Otieno katika kipindi cha kwanza na cha pili mtawalia.

kra

Ushindi huo unawapaisha matarishi hadi nafasi ya pili kwa alama alama 29 kutokana na mechi 16, pointi 2 nyuma ya mabingwa watetezi Gor Mahia walio na mchuano mmoja mkobani.

Katika mikwangurano mingine  ya Alhamisi, Nzoia Sugar imewabwaga KCB bao moja kwa sifuri uwanjani Police Sacco, Mohammed Barisa akiwa mfungaji.

Kariobangi Sharks imeititiga  Talanta FC mabao matatu kwa bila kiwarani Kenyatta kaunti ya Machakos, Geofrey Onyango, Keith Imbali na Stanley Wilson wakibusu nyavu mara moja kila mmoja.

Shabana Fc wameambulia kichapo cha goli moja kwa bila katika uwanja wa manispaa wa Thika dhidi ya wenyeji Bidco United.

Mechi mbili za kuhitimisha raundi ya 16 zitapigwa Ijumaa, Gor Mahia wakiikaribisha Bandari FC uwanjani Machakos nao Kakamega Homeboyz wachuane na Nairobi City Stars katika uchanjaa wa Bukhungu.

 

Website | + posts