Home Habari Kuu Matabibu watoa ilani ya mwezi mmoja ya mgomo

Matabibu watoa ilani ya mwezi mmoja ya mgomo

0

Matabibu wametoa ilani ya mwezi mmoja kabla ya kuanza mgomo wa kitaifa kufuatia, kufutiliwa mbali kwa bima yao ya matibabu iliyokuwa katika bima ya NHIF.

Kwenye arifa hiyo madaktari kupitia kwa chama chao cha KMPDU kimeapa kugoma ikiwa wizara ya afya haitarejesha bima  ya matibabu, waliyokuwa wakipokea kupitia huduma ya bima ya NHIF au bima mpya ya SHIF.

Wizara ya afya ilisitisha bima hiyo kwa matabibu bila kutoa sababu zozote, huku madaktari wakilalama kuwa wamekuwa wakitaabika kupata huduma za matibabu.

KMPDU inataka bima yao ya matibabu ijumuishwe katika huduma mpya ya SHIF la sivyo waitishe mgomo wa kitaifa kuanzia mwezi Machi.

Website | + posts