Home Michezo Mason Mount ni nani? Mfahamu kiungo nyota mpya wa klabu ya Manchester...

Mason Mount ni nani? Mfahamu kiungo nyota mpya wa klabu ya Manchester United

Katika kumsajili Mason Mount, United wametoa ilani ya nia ya kuanza msimu kwa ubora zaidi chini ya mkufunzi Erik Ten Hag.

0

Mason Tony Mount alizaliwa Januari tarehe 10 mwaka wa elfu moja Kenda mia tisini na tisa 1999, Katika Mji wa Portsmouth Nchini Uingereza.

Maisha ya Kandanda ya kijana mdogo (Mount) kutoka Portsmouth yalianza kwenye shule ya kunoa makali na kukuza talanta za wachezaji kinda, (academy) ya Chelsea Cobham kuanzia mwaka wa 2005 Hadi 2017 ambayo ilimnoa na kutimiza ndoto yake ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Mwaka wa 2017 Mount alipandisha ngazi kutoka kwa Academy ya Klabu hiyo na kujiunga na timu ya wakubwa (first team) japo alianza kwa kupelekwa Katika vilabu vingine Ili kusaidia ukuaji wake.

Mason Mount ambaye ana umri wa miaka (24) kwa sasa ni mchezaji wa kiungo cha kati (Central midfielder) au Kiungo Mshambuliaji ( attacking midfielder).

Msimu wa 2017-2018 Mason Mount alipopandishwa hatua Stamford Bridge, alijiunga na klabu ya Vitesse kwa mkopo na kuichezea klabu hiyo ya Uholanzi mechi 29 na kufunga magoli 9 tu, msimu wa 2018-2019 Mount alijiunga na Derby county kwa mkopo akicheza mechi 35 na kufunga magoli 8 kisha kurudi tena kwenye klabu ya Chelsea mwaka huo wa 2019 chini ya Kocha Frank Lampard ambaye msimu uliokamilika wakati akiinoa Chelsea Lampard alimtaja Mount kuwa mchezaji mwenye uelewe mkubwa na mwerevu wa mchezo wa Kandanda.

“Kitu cha kwanza ambacho mchezaji wa kiwango Cha juu anapaswa kuwa nacho ni hamu na njaa ya kweli ya kufanikiwa na kucheza na kufanya vyema kwa Chelsea, na Mount amekuwa nayo tangu siku ya kwanza nilipompeleka Derby County kwa mkopo. Hiyo ni rahisi kwangu. Bado ni mchezaji mchanga. Anaweza kwenda mbali zaidi lakini tayari ni mchezaji bora.” Aliyekuwa Kocha wa Chelsea Frank Lampard aliambia wanahabari mwaka huu alipoulizwa kuhusu kiwango Cha Mason Mount kushuka.

Akiwa na Chelsea Mount amefanikiwa kushinda kushinda Kombe la klabu BINGWA ulaya (Uefa champions League), Uefa super cup na FIFA Club World Cup, ikiwa ni pamoja na kushinda taji la mchezaji bora wa klabu ya Chelsea msimu wa 2020-2021 na msimu wa 2021-2022 kwa mfululizo.

Mason Mount akishangilia baada ya kushinda tuzo la klabu BINGWA ulaya na klabu ya Chelsea.

Kwa jumla Mason Mount amechezea klabu ya Chelsea mechi 195 na kufunga magoli 33, vile vile tangu mwaka wa 2019 Mount amesaidia magoli 22 (assists) Katika kiwango Cha mashindano ya Klabu

Mason Mount aliwahi kushinda tuzo la Uefa European kwa kikosi chini ya miaka 19 akiwa na timu ya Taifa ya Uingereza kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 19( under 19 ) mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 20 alitajwa Katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ya wakubwa na alikuwa kwenye kikosi kilichocheza Uefa Euro 2020 pamoja na michuano ya kombe la dunia 2022 kule Qatar.

Klabu ya Manchester United ilimsajili Mount kutoka Chelsea kwa day la pauni milioni 60.

Mason Mount ni mmoja kati ya viungo wenye vipaji na anapojiunga na Vijana wa Erik Ten Hag ambae amekuwa akihitaji saini yake kwa lengo la kuboresha kikosi chake tunapoingia msimu ujao hasa kwenye eneo la kiungo, ni wazi kwamba atakuwa wa muhimu sana Katika kuimarisha safu ya mashambulizi na Kati.

Kwa namna ambavyo anacheza Mason Mount anaweza kuongeza kitu kwenye eneo hilo na ndio maana Manchester United wametumia £60m kuhakikisha wanapata saini ya kiungo huyo muingereza.

Katika kumsajili Mason Mount, United wametoa ilani ya nia ya kuanza msimu kwa ubora zaidi chini ya mkufunzi Erik Ten Hag ambaye aliwaongoza Vijana wake kushinda kikombe Cha -Carabao Cup baada ya klabu hiyo ya Old Trafford kukawia tuzo lolote kwa kipindi cha miaka sita na kuwarejesha kwenye mashindano ya Ligi ya klabu bingwa ulaya

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here