Home Habari Kuu Masomo yasimamishwa KU kuwaomboleza wanafunzi waliofariki

Masomo yasimamishwa KU kuwaomboleza wanafunzi waliofariki

Wanafunzi hao walikuwa wakielekea Mombasa kwa ziara ya kimasomo, ajali hiyo ilipotokea.

0

Chuo Kikuu cha Kenyatta, KU  kimesimamisha masomo kwa muda wa siku tatu ili kutoa fursa ya kuomboleza wanafunzi waliofariki katika ajali ya barabarani Jumatatu usiku.

Katika taarifa siku ya Jumanne, Naibu Chansela wa chuo hicho alisema shughuli za masomo zitasitishwa kwa siku tatu kuanzia tarehe 20 hadi 24 mwezi huu.

“Kufuatia ajali iliyotokea, usimamizi wa chuo umesimamisha masomo kwa siku tatu kuanzia Jumatano tarehe 20, kutoa fursa ya kuwaomboleza wanafunzi waliofariki,” ilisema taarifa ya chuo hicho.

Hayo yalijiri huku wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo wakisafirishwa kwa ndege hadi jijini Nairobi kupokea matibabu maalum.

Juzi Jumatatu usiku, basi la Chuo Kikuu cha Kenyatta liligongana na lori katika eneo la Maungu, Voi katika kaunti ya Taita Taveta.

Wanafunzi hao walikuwa wakielekea Mombasa kwa ziara ya kimasomo, ajali hiyo ilipotokea.

Wanafunzi 11 waliripotiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Website | + posts