Home Habari Kuu Masomo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yajumuishwa kwenye mtaala

Masomo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yajumuishwa kwenye mtaala

0

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema wizara yake imeweka masomo kuhusu namna ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi kwenye mtaala.

Waziri Machogu anasema kwamba kupitia kwa masomo hayo, wanafunzi wanapata ujuzi kuhusu mwonekano wa mazingira na jinsi wanaweza kulinda mazingira kwa njia ya uvumbuzi na endelevu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa haki ya mabadiliko ya hali ya hewa, Machogu alisema masomo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yanahusu wanafunzi kuhusika kwenye mipango kama upandaji wa miti.

Kulingana naye, wizara imeandaa mafunzo kwa waalimu ili kuongeza ujuzi wao katika maswala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Machogu alisema elimu ni chombo muhimu katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa muungano wa haki ya tabianchi Afrika Daktari Mithika Mwenda alisema kuwapa waafrika wa umri mdogo elimu na vifaa vya kuendeleza suluhisho la kudumu ndiko kunastahili kupatiwa kipaumbele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here