Home Habari Kuu Mashua za kibinafsi zaruhusiwa kuhudumu Garissa

Mashua za kibinafsi zaruhusiwa kuhudumu Garissa

Mashua hizo za kibinafsi zitaruhusiwa kuwabeba watu 10 kwa wakati mmoja, nauli ikiwa shilingi 200.

0
Mashua za kibinafsi zaruhusiwa kuhudumu Garissa.

Mashua za kibinafsi katika eneo la Garissa na Madogo, zimeruhusiwa kuwasafirisha watu katika barabara iliyofurika ya Garissa – Madogo, chini ya usimamizi wa huduma ya taifa ya polisi.

Kulingana na naibu kamishna wa kaunti ya Bangale Joseph Kipkorir, mashua hizo za kibinafsi zitaruhusiwa kuwabeba watu 10 kwa wakati mmoja, nauli ikiwa shilingi 200.

Wahudumu wa mashua hizo hata hivyo, wametakiwa kuwapa abiria mavazi ya usalama, huku abiria hao wakihitajika kusajili maelezo yao katika kituo cha ushirikishi kilichobuniwa, kabla ya kuabiri mashua hizo.

“Kuna watumishi wa umma hapa wanaofanya kazi Garissa, pamoja na maafisa wa polisi au wale ambao wanashughulikia maswala ya dharura. Tunaruhusu makundi hayo ya watu kusafiri,” alisema naibu huyo kamishna wa kaunti.

Hapo awali mashua hizo zilikuwa zikiwabeba abiria kupita kiasi huku zikiwatoza abiria nauli ya shilingi 1500. Wahumudu wa mashua hizo pia hawakuzingatia kuvalia mavazi ya usalama.

Website | + posts