Takriban wahamiaji 200 kutoka Senegal, hawajulikani waliko baada ya boti walimokuwa wakisafiria kutoweka katika visiwa vya Canary, huku shughuli za uokoaji zikiendelea.
Waokoaji wa Uhispania wanajizatiti kuwatafuta wahamiaji hao kutoka Afrika ya kati, ambao inasemekana walitoweka zaidi ya wiki moja iliyopita.
Kundi la misaada la Walking Borders linasema mashua hiyo ya wavuvi, ilisafiri kutoka Kafountine, mji wa pwani kusini mwa Senegal ambao uko takriban kilomita 1,700 kutoka Tenerife.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Efe la Uhispania, watoto wengi wako katika boti hiyo.
Boti mbili sawia zilizobeba makumi ya watu zaidi pia zinasemekana kupotea.