Home Habari Kuu Mashirika ya umma yatakiwa kuwaajiri walemavu zaidi

Mashirika ya umma yatakiwa kuwaajiri walemavu zaidi

0

Mashirika ya umma yametakiwa kuwaajiri zaidi walemavu,ili kuafikia asililimia tano ya wafanyikazi walemavu inavyohitajika kikatiba.

Waziri wa Leba Florence Bore aliyehudhuria uzinduzi wa ripoti ya pili kuhusu ujumuishaji wa walemavu katika afisi za umma mwaka 2022/2023, alitoa changamoto kwa mashirika yote ya umma kusoma na kutathmini ripoti hiyo na kuitekeleza.

Kwa mjibu wa ripoti hiyo ni asilimia 1.2 pekee ya mashirika ya serikali yamewaajiri walemavu dhidi ya hitaji la kikatiba la asilimia 5.

Ripoti hiyo iliyotolewa Alhamisi pia ilifichua kuwa ni mashirika 129 pekee ya serikali kati ya mashirika yote 240, yamewaajiri walemavu ikijumuisha idara za serikali 369 kati ya idara zote 418.

Kadhalika ripoti hiyo ilifichua kuwa ni mashirika 13 pekee ya serikali yametimiza kuwaajiri walemavu asilimia 5 ,huku mengine 116 yakiwa na wafanyikazi walemavu chini ya kiwango kinachohitajika.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika la wamavu nchini Harrun Hassan, ametoa changamoto kwa mashirika yaliyosalia kutoa vikwazo na kuwapa fursa wafanyikazi walemavu .

Website | + posts