Home Habari Kuu Mashirika ya umma yatakiwa kutowalipa maafisa walioajiriwa na stakabadhi ghushi

Mashirika ya umma yatakiwa kutowalipa maafisa walioajiriwa na stakabadhi ghushi

0

Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini (EACC), imetoa arifa kwa taasisi zote za serikali ya kitaifa na zile za kaunti, kusimamisha malipo kwa wafanyakazi wote wanaojiuzulu kutoka huduma ya umma au wale wanaostaafu mapema ndio kukwepa uchunguzi unaoendelea wa visa vya kughushi stakabadhi za masomo.

Tume hiyo pia imewaagiza maafisa wote wakuu wasimamizi wa taasisi hizo, kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wa umma walioajiriwa kwa kutumia hati ghushi za masomo wanarejesha mishahara yote na marupurupu waliyolipwa.

Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbarak, alisema katika baadhi ya visa hivyo,washukiwa wa kutumia hati ghushi walishirikiana na maafisa wakuu wa hesabu za pesa kulipwa marupurupu yao ya kustaafu au baada ya kujiuzulu.

Mnamo mwezi Februari, tume ya kuwaajiri watumishi wa umma ilifichua kwamba zaidi ya watumishi elfu mbili wa umma waliajiriwa, kupandishwa vyeo au kubadilisha majukumu yao kwa kutumia hati ghushi za masomo.

Website | + posts