Home Michezo Mashindano ya Safaricom Chapa Dimba kuelekea Siaya na Kisii

Mashindano ya Safaricom Chapa Dimba kuelekea Siaya na Kisii

Mabingwa kwa wavulana na wasichana watatuzwa shilingi 75,000 na shilingi 30,000 kwa wale watakaomaliza nafasi ya pili .

0

Mashindano ta Safaricom Chapa Dimba yataelekea katika kaunti za Siaya na Kisii mwishoni mwa juma hili .

Siku ya Jumamosi kaunti ya Siaya itaandaa mashindano yake katika uwanja wa chuo cha matibabu Jera Girls ya Ugenya na VSA Girls ya Gem, zikipambana katika fainali wakati ile ya wavulana ikiwa baina ya Ambira Mobimba ya Ugunja dhidi ya St. Peter’s Wagai Mixed Secondary ya Gem.

Jumapili , Kisii Queens wwatapambana dhidi ya Moteiribe FC ya Kenyenya huku Small Simba ikikabana koo na Ichuni FC katika uwanja wa Sameta ,kaunti ya Kisii.

Mabingwa kwa wavulana na wasichana watatuzwa shilingi 75,000 na shilingi 30,000 kwa wale watakaomaliza nafasi ya pili .

Mashindano ya eneo la Nyanza yataandaliwa Oktoba mosi mwaka huu huku eneo hilo likitoka timu zaidi ya 530 zilizojiandikisha kushiriki.

Website | + posts