Home Habari Kuu Mashindano ya riadha ulimwenguni yaanza Budapest

Mashindano ya riadha ulimwenguni yaanza Budapest

0

Kenya itakuwa ikiwinda nishani kwenye fainali tatu katika siku ya kwanza ya makala ya 19 ya mashindano ya riadha duniani mjini Budapest, Hungary leo Jumamosi.

Fainali ya kwanza itakuwa matembezi ya kilomita 20 kwa wanaume kuanzia saa nne kasoro dakika 10 asubuhi.

Bingwa mara tatu wa Afrika Samuel Gathimba Ireri atajitosa kwenye fainali hiyo akiwa Mkenya pekee akijaribu kuzoa medali baada ya kukosa katika makala ya mwaka uliopita mjini Oregon nchini Marekani.

Saa sita na dakika 5, kutakuwa na mchujo wa mita 400 kwa wanariadha wanne mseto kupokezakana kijiti huku fainaki yake ikianza saa nne na dakika 47 usiku.

Agnes Jebet Ngetich, Irene Kimais na Grace Loibach watatimka fainali ya mita 10,000 kuanzia saa tatu na dakika 47 usiku.

Mashindano mengine kwa Wakenya ni raundi ya kwanza ya mita 1,500 kwa wanaume na wanawake na raundi ya kwanza ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Kenya ilizoa medali 10 katika makala ya mwaka jana nchini Marekani kwa dhahabu 2, fedha 5 na shaba 3.

Mashindano hayo yatakayokamilika Agosti 27 yatapeperushwa mubashara na runinga ya taifa ya KBC Channel 1.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here