Home Habari Kuu Masaibu ya mafuriko Tana River, familia 27,000 zaathirika

Masaibu ya mafuriko Tana River, familia 27,000 zaathirika

0

Jumla ya 27,000 zimeathiriwa na mafuriko katika kaunti ya Tana River. 

Familia zaidi ya 38,000 zimeathiriwa na mafuriko katika eneo la Pwani.

Shirika la Msalaba Mwekundu linasema jumla ya kaunti sita zimeathiriwa mno na mafuriko katika ukanda wa Pwani.

Katika kaunti ya Tana River, wakazi wamelazimika kuhama makwao baada ya nyumba zao kufurika maji ya mafuriko.

Waathiriwa wamelazimika kuacha nyuma mali zao zilizofunikwa na maji.

Mvua kubwa zinazonyesha nchini zimesababisha mafuriko katika maeneo kadhaa nchini huku jumla ya kaunti 38 kati ya 47 zikiathirika vibaya.

Watu zaidi ya 100 wamefariki kutokana na mafuriko hayo.

Serikali inasema imeweka hatua madhubuti za kukabiliana na mafuriko hayo.

 

 

 

Website | + posts