Home Burudani Marufuku dhidi ya mwigizaji Jerry Williams yaondolewa

Marufuku dhidi ya mwigizaji Jerry Williams yaondolewa

0

Chama cha waigizaji nchini Nigeria almaarufu Actors Guild of Nigeria – AGN kimeondoa marufuku iliyowekwa dhidi ya mwigizaji Jerry Williams.

Uanachama wa Williams kwenye AGN ulisimamishwa Juni 28, 2023 kutokana na kile kilichotajwa kuwa matumizi ya mihadarati kinyume cha katiba ya chama.

Rais wa kitaifa wa chama cha AGN Emeka Rollas alitoa taarifa akielezea kwamba waliamua kusimamisha uanachama wa Jerry ili kuhakikisha kwamba hahatarishi maisha ya waigizaji wenza wakiwa kazini.

Alipelekwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia ili kupata usaidizi wiki kadhaa zilizopita, na sasa uongozi wa chama hicho cha waigizaji umetangaza kwamba Jerry amerejeshwa chamani.

Mwigizaji huyo alichapisha video kwenye akaunti yake ya Instagram ambapo anasikika akisema marufuku dhidi yake imeondolewa na anarejea kazini kuigiza.

Alitoa shukrani kwa wote ambao wamemsaidia katika safari yake ya urekebishaji tabia na kurejelea maisha ya kawaida akiwemo Rais wa AGN Emeka Rollas na mwigizaji mwenza Destiny Etiko kati ya wengine wengi.

Jerry Williams ambaye anasemekana kuzamia uraibu wa mihadarati kutokana na msongo wa mawazo alionekana mwenye siha njema na aliahidi mashabiki wake filamu nzuri nzuri kutoka sasa.

Uongozi wa AGN ulielezea kwamba Williams alishirikiana nao ndio maana marufuku dhidi yake iliondolewa.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here