Home Habari Kuu Maribe kuongoza mawasiliano katika afisi ya Waziri Kuria

Maribe kuongoza mawasiliano katika afisi ya Waziri Kuria

0

Jackie Maribe ambaye alikuwa msomaji wa habari katika runinga na ripota ameteuliwa kuhudumu kama mkuu wa shughuli za mawasiliano katika wizara ya utumishi wa umma.

Wizara hiyo inasimamiwa na waziri Moses Kuria na uteuzi huu unajiri siku kadhaa baada ya Maribe kuondolewa lawama kwenye kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani.

Rafiki ya Maribe Dennis Itumbi alitangaza uteuzi huo kupitia kumpongeza kwenye akaunti yake ya mtandao wa X akimtakia baraka na kila la kheri katika kazi hiyo mpya.

Alimshukuru waziri Kuria pia kwa kile alichokitaja kuwa kusimama na kizazi huku akimshauri aendelee kufanya mema na kunyosha mkono kusaidia watu.

Kesi ya mauaji ya Monica Kimani imekuwa ikiendelea kwa muda wa miaka sita na Februari 9, 2024 jaji Grace Nzioka alimwondolea lawama Maribe kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kuonyesha alihusika.

Mshtakiwa mweza Jowie Irungu hata hivyo alipatikana na hatia ya kumuua Kimani na anasubiri kuhukumiwa. Hapo jana mahakama iliahirisha utoaji wa hukumu hiyo.

Website | + posts