Home Habari Kuu Maribe, Jowie kujua hatima Ijumaa

Maribe, Jowie kujua hatima Ijumaa

0
Jackie Maribe na Joshua Irungu, kujua hatma yao tarehe 15 Disemba.

Mwanahabari Jackie Maribe na mpenziwe wa zamani Joshua Irungu, maarufu kama Jowie, wanatarajiwa kubaini hatima ya kesi ya mauji inayowakabili ya mfanyabiashara wa kike Monica Kimani siku ya Ijumaa.

Jaji wa mahakama kuu Grace Nzioka anatarajiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo ambayo imekuwa mahakamani kwa muda mrefu.

Maribe na Jowie wanashukiwa kuhusika katika mauaji ya Kimani mwaka 2018, mashtaka ambayo wameyakanusha mara kadhaa huku wakiachiliwa kwa dhamana.

Jowie ndiye mshukiwa mkuu huku huku Maribe akishtakiwa kwa kuwa msaidizi katika mauaji hayo.

Kesi hiyo ilikuwa iamuliwe mwezi Julai mwaka uliopita lakini uamuzi ukaahirishwa hadi Oktoba mwaka huo, kufuatia kuugua kwa jaji Nzioka.

Mashahidi 35 walitoa ushahidi wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Marehemu Kimani alipataikana ameuawa katika makao yake ya Lamuria Gardens, karibu na barabara ya Dennis Pritt mwaka 2018 mtaani Kilimani.

Website | + posts