Home Kimataifa Marekani yatoa msaada wa kibinadamu Gaza

Marekani yatoa msaada wa kibinadamu Gaza

0

Marekani imesambaza msaada wa kwanza wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza ambapo vyakula vilivyopakiwa vinavyotosha zaidi ya watu elfu 30, vikisambazwa kwa kutumia ndege tatu za kijeshi.

Oparesheni hiyo ilitekelezwa kwa ushirikiano na jeshi la wanahewa la Jordan na ndiyo ya kwanza kati ya nyingi zilizotangazwa na Rais Joe Biden.

Aliahidi kuongeza msaada baada ya watu wapatao 112 kufariki wakati umati wa watu ulikimbilia magari ya msaada Alhamisi.

Haya yanajiri wakati ambapo kiongozi mmoja wa ngazi za juu katika serikali ya Marekani amedokeza kwamba mfumo wa muda wa wiki sita wa kusitisha mapigano katika eneo hilo umeafikiwa.

Afisa huyo alisema jana Jumamosi kwamba Israel imekubali mfumo huo wa kusitisha mapigano ambao ungeanza jana iwapo wanamgambo wa kundi la Hamas wangekubali kuachilia mateka wa Israel walio hatarini kama wagonjwa, waliojeruhiwa, wakongwe na wanawake.

Wapatanishi wanakutana jijini Cairo nchini Misri ambapo wawakilishi wa Hamas na Israel wanatarajiwa kufika kwa ajili ya majadiliano.

masuala yanayohitaji kutatuliwa kabla ya kuanza kutekeleza mpango huo wa kusitisha mapigano ni kama idadi ya wafungwa wapalestina watakaoachiliwa na Israel kubadilishana na wanaoshikiliwa na Hamas.

Website | + posts