Home Habari Kuu Marekani yatangaza muungano wa kimataifa kulinda meli katika Bahari Nyekundu

Marekani yatangaza muungano wa kimataifa kulinda meli katika Bahari Nyekundu

0
kra

Serikali ya Marekani imetangaza muungano wa kimataifa utakaozingatia usalama katika Bahari Nyekundu, kufuatia msururu wa mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara.

Katika taarifa yake, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin anasema “mashambulizi ya kiholela ya Houthi” kutoka Yemen dhidi ya meli “yanatishia mtiririko huru wa biashara, kuhatarisha maiasha ya mabaharia wasio na hatia, na yanakiuka sheria za kimataifa”.

kra

Makampuni kadhaa makubwa ya meli yamesitisha shughuli zake katika eneo hilo kufuatia msururu wa mashambulizi dhidi ya meli katika mlango wa Bab al-Mandab na wanamgambo wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran katika siku na wiki za hivi karibuni.

“Bahari Nyekundu ni njia muhimu ya maji ambayo imekuwa muhimu kwa uhuru wa urambazaji na ukanda mkubwa wa kibiashara unaowezesha biashara ya kimataifa,” anasema

Njia hiyo ya meli inaunganisha meli zinazotoka Asia na Afrika mashariki hadi Ulaya kupitia Mfereji wa Suez nchini Misri, ambao ndio sehemu kuu ya kufikia Bahari ya Mediterania kwa meli zinazosafiri kutoka Bahari ya Hindi.

Nchi ambazo “zinatafuta kushikilia kanuni ya msingi ya uhuru wa urambazaji”, Austin anasema, lazima zifanye kazi pamoja ili kuzuia Houthis kurusha makombora ya balestiki na ndege zisizo na rubani kwenye meli za kibiashara katika maji ya kimataifa kutoka Yemen.

Anaongeza ujumbe huo uliopewa jina la Operesheni Prosperity Guardian, utajumuisha Uingereza, Bahrain, Canada, Ufaransa, Italia, Uholanzi, Norway, Ushelisheli na Uhispania.

BBC
+ posts