Home Habari Kuu Marekani yatambua juhudi za Kenya za kuleta amani upembe wa Afrika

Marekani yatambua juhudi za Kenya za kuleta amani upembe wa Afrika

0

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amepongeza mchango wa Kenya wa kuleta amani na udhabiti katika upenbe wa Afrika na ulimwengu kwa jumla.

Blinken alisema Kenya, chini ya uongozi wa Rais William Ruto, imekuwa nguzo muhimu katika maswala ya amani na usalama katika Kanda hii.

Wakati huo huo Blinken alipongeza Kenya kwa kukubali kuwatuma maafisa wa usalama nchini Haiti.

Blinken alitambua  juhudi za Kenya katika kushughulikia changamoto za usalama katika kanda hii hasa katika maeneo ya kaskazini mwa Ethiopia, mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Sudan kusini na Somalia.

Blinken aliyasema hayo alipokutana na Rais William Ruto Jijini New York Marekani.

Kwa upande wake Rais William Ruto alishukuru Marekani kwa kushiriki katika kongamano kuhusu tabia nchi na Kwa mchango wake wa dola milioni 30 kuhakikisha usalama wa chakula barani Afrika.

Aidha Rais alisema kenya inatafuta fursa mpya za uwekezaji na biashara na Marekani..

Website | + posts