Home Habari Kuu Marekani yashutumu ukatili wa vikosi vya RSF nchini Sudan

Marekani yashutumu ukatili wa vikosi vya RSF nchini Sudan

0
kra

Marekani imelaani vitendo vya ukatili vinavyodaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji la Rapid Support Forces (RSF) na wanamgambo washirika katika eneo la Darfur Magharibi nchini Sudan ambavyo ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na mauaji ya kikabila.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani inasema huku ukatili huo ukitekezwa na RSF na wanamgambo washirika, pande zote mbili katika mzozo huo zinahusika na unyanyasaji.

kra

Wizara hiyo inasema kuwa jeshi la Sudan lilishindwa kuwalinda raia na lilichochea vita katika eneo hilo kwa kukuza uhasama wa kikabila.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mashauri ya kigeni wa Marekani Mathew Miller kwenye taarifa yake, ukatili unaotokelezwa huko Darfur Magharibi na maeneo mengine ni ukumbusho wa kutisha wa matukio ya kikatili ambayo yalisababisha Marekani kubaini kwamba mnamo mwaka 2004 mauaji ya halaiki yalitekelezwa huko Darfur.

Taarifa hiyo ilitolewa baada ya jeshi la Sudan kushutumu wapiganaji wa RSF kwa “kumteka nyara na kumuua” gavana wa Darfur Magharibi, Khamis Abdalla.

Hata hivyo, kundi la RSF limekanusha dai hilo.Takriban watu alfu moja wameuawa katika mashambulizi ya makundi yanayounga mkono kundi la RSF huko Darfur Magharibi, kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu nchini Sudan.

Mapigano kati ya Jeshi la Sudan na kundi RSF, ambayo yalizuka tarehe 15 Aprili, yanakadiriwa kuchangia zaidi ya watu milioni mbili kutoroka makwao.

Website | + posts