Home Habari Kuu Marekani yasema kampuni ya Crown Bus inafadhili Al-Shabaab

Marekani yasema kampuni ya Crown Bus inafadhili Al-Shabaab

0

Marekani imeorodhesha kampuni na watu wanaotuhumiwa kufadhili kundi la kigaidi la Al- Shabaab kupitia ulanguzi wa fedha.

Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na kampuni moja ya Kenya ya uchukuzi wa umma ya Crown Bus, ambayo imetajwa na Marekani kuwa inasaidia kundi hilo kupitia operesheni za uchukuzi.

Kupitia kwa taarifa siku ya Jumatatu, Marekani ilisema watu hao ni miongoni mwa mtandao mkubwa wa biashara kutoka upembe wa Afrika, Umoja wa Milki za Kiarabu na Cyprus, ambazo hukusanya fedha kwa niaba ya Al-Shabaab.

Taarifa hiyo ilisema Al-Shabaab hukusanya dola milioni 100  kila  mwaka kupitia biashara na watu binafsi wanaofungamana na kundi hilo.

“Serikali ya Marekani imejitolea kushirikiana na washirika wa kanda kuangamiza wanaofadhili shughuli za ugaidi,” ilisema taarifa hiyo.