Home Kimataifa Marekani yaonya Korea Kaskazini dhidi ya kuuzia Urusi silaha

Marekani yaonya Korea Kaskazini dhidi ya kuuzia Urusi silaha

0

Mshauri wa ngazi za juu katika ikulu ya White House amesema kwamba Korea Kaskazini italipia iwapo itauzia Urusi silaha za kutumia katika vita nchini Ukraine. Haya yanajiri baada ya Marekani kuonya kwamba Korea Kaskazini ilikuwa ikifanya mazungumzo na Urusi kuhusu uwezekano wa mpango huo wa silaha.

Jake Sullivan mshauri wa serikali ya Marekani kuhusu usalama alisema Jumanne kwamba Marekani inaamini mashauriano kati ya Korea Kaskazini na urusi yanaendelea kwa kasi.

“Kuipatia Urusi silaha kutumia kushambulia maghala ya nafaka huku joto likiongezeka kwenye miundomsingi tunapoelekea majira ya baridi kujaribu kunyakua himaya ya taifa huru, hili halitakuwa zuri kwa upande wa Korea Kaskazini na watalipa gharama kwa jamii ya kimataifa.” alisema Sullivan katika kikao na wanahabari.

Matamshi yake yanajiri baada ya afisa mwingine wa serikali ya Joe Biden kusema Jumatatu kwamba Marekani ilikuwa inatarajia rais wa Korea Kaskazini Kim Jong kufanya mkutano namwenzake wa Urusi Vladimir Putin.

Ikulu ya Rais nchini Uturuki almaarufu Kremlin haijatoa tamko lolote kuhusu madai ya Marekani ikisisitiza kwamba haina la kusema.

Dalili za kuimarika kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili zimekuwa zikidhihirika hadharani katika muda wa wiki chache zilizopita.

Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alizuru Korea kaskazini ambapo alikutana na Rais Kim Jong Un mwezi Julai. Marais Kim na Putin nao walibadilishana nyaraka mwezi jana wakiahidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao.

Website | + posts