Home Kimataifa Marekani kutoa misaada zaidi kwa Ukraine

Marekani kutoa misaada zaidi kwa Ukraine

0

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, ametangaza msaada mpya wa kijeshi wa dola milioni 100 kwa Ukraine.

Ametangaza hayo wakati wa ziara ambayo haikutangazwa ya Kyiv, Jumatatu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwahakikishia viongozi wa Ukraine kwamba Marekani itaendelea kuunga mkono mapambano ya nchi hiyo dhidi ya uvamizi wa Russia.

Baada ya safari ya treni ya usiku kutoka Poland, waziri Austin, alikutana na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky mjini Kyiv, ambaye alimshukuru waziri wa ulinzi wa Marekani.

Rais Zelenskyy amesema kwenda kwa waziri huyo ni ishara muhimu sana kwa Ukraine, na kuongeza kwamba anaishukuru sana Marekani, pamoja kwamba wako pamoja na Ukraine, katika matatizo yote na kipindi kigumu cha miaka yote.

Msaada wa ziada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine unatokana na hifadhi zilizopo za silaha na unajumuisha mizinga, mifumo ya ulinzi wa anga na mingine ya roketi za juu, au HIMARS

Website | + posts
VOA
+ posts