Home Biashara Marekani kushirikiana na kampuni ya Kenya kuinua sekta ya nazi

Marekani kushirikiana na kampuni ya Kenya kuinua sekta ya nazi

0
kra

Marekani imetangaza ushirikiano na kampuni moja inayojihusisha na utayarishaji bidhaa kutokana na nazi kwa jina Kentaste, ambao utapanua fursa za kiuchumi kwa wakulima wapatao 4500 wa Kenya.

Balozi Meg Whitman alitangaza ushirikiano huo Jumatatu Agosti 28, 2023 akiwa na wasimamizi wa kampuni ya Kentaste ambapo alisema kwamba mradi huo ambao umefadhiliwa na shirika la USAID na Kentaste wa dola milioni 1.6 sawa na milioni 232,400,000 za Kenya utaimarisha juhudi za wakulima kuongeza bidhaa za Kenstate zinazouzwa katika soko la Marekani.

kra

Marekani inapiga jeki mradi huo kupitia kwa shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID chini ya mpango uitwao “Feed the Future and Prosper Africa” yaani “lisha vizazi vijavyo, fanikisha Afrika.

Uzalishaji katika kampuni ya Kentaste utaongezeka kwa kiwango cha asilimia 67 hadi nazi elfu 50 kwa siku na kutoa nafasi 90 za ajira ya kudumu kando na kusajili wakulima wengine wapya 1,500 kama wasambazaji wa malighafi. Asilimia 30 ya wakulima hao wapya watakuwa wanawake.

Hasara ya lita 32,500 za chakula na nyingine itatokomezwa kupitia kuboresha usindikaji.

Balozi Whitman alisema wanaimarisha biashara, kubadilisha maisha ya watu na kukabiliana na uharibifu wa chakula kupitia ushirikiano kama huo.