Home Habari Kuu Marais watatu kuhudhuria sherehe za Jamhuri

Marais watatu kuhudhuria sherehe za Jamhuri

Rais wa Belarus Aleksandr Lukashenko, Rais  Félix Tshisekedi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,  na Rais wa Ethiopia Sahle Work Zewde tayari wamewasili hapa nchini.

0

Taifa hili linapoadhimisha miaka 60 ya uhuru, Marais watatu watahudhuria sherehe hizo zitakazoandaliwa katika bustani ya Uhuru Gardens leo Jumanne.

Rais wa Belarus Aleksandr Lukashenko, Rais  Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rais wa Ethiopia Sahle Work Zewde tayari wamewasili hapa nchini, wakiwa wageni wa Rais William Ruto katika sherehe hiyo.

Raia wa Ethiopia Sahle-Work Zewde, awasili katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Rais wa Ethiopia na ujumbe wake walilakiwa jana Jumatatu katika uwanja wa ndege wa kitaifa wa Jomo Kenyatta na Waziri wa Biashara na Viwanda Rebecca Miano.

Awali, Rais Lukashenko alifanya mazungumzo na Rais Ruto katika Ikulu ya Nairobi, ambapo viongozi hao wawili walikubaliana kuboresha uhusiano wa nchi hizi mbili hasa katika sekta za nishati, biashara, uwekezaji na elimu.

Website | + posts