Home Michezo Mancity watafunwa na mbweha huku Man U wakiduwazwa

Mancity watafunwa na mbweha huku Man U wakiduwazwa

0

Rekodi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza Manchester City,kutopoteza msimu huu ilivunjwa baada ya kuambulia kichapo cha magoli mawili kwa moja ugenini mikono ni mwa Wolverhampton Wanderers ugani Moleneux.

Reuben Diaz alijipiga goli mwanzoni mwa mechi kabla ya Julian Alvarez kusawazisha kipindi cha pili lakina Hwang Lee apiga goli kwa mbweha wakipata ushindi adimu.

Katika matokeo mengine Manchester United ilifadhaishwa nyumbani ikipigwa na vijana wa kasri Crystal Palace moja kwa nunge huku Arsenal wakiigaragaza Bournemouth mabao manne kwa ombwe.

Website | + posts