Home Michezo Mancity na Man U kukabana koo fainali ya FA

Mancity na Man U kukabana koo fainali ya FA

0

Mabingwa watetezi wa kombe la FA na ligi kuu ya Uingereza Manchester City watawakabili mahasimu wao Manchester United leo jioni ugani Wembley kwenye fainali ya taji la FA.

Itakuwa fursa ya Man United kulipiza kisasi cha mwaka jana waliposhindwa mabao mawili Kwa Moja.

Manchester City watakuwa wanawinda taji la nane na wanakabiliwa na jereha la mlinda lango Ederson Santana de Moraes pekee ambaye atakosa mechi hiyo.

Red devils ambao walimaliza wa nane kwenye ligi kuu, watakuwa wanawinda taji la 13 huku wakikabiliwa na majeraha chungu tele ikiwemo ya kiungo Mason Mount, Harry Maguire, Victor Lindelof, Tyrell Malacia, Anthony Martialna Luke Shaw.

Iwapo mukufunzi wa City Pep Guardiola atashinda,litakuwa taji la 18 tangu achukue hatamu za uongozi 2016.

Kwa upande wa Erik ten Hag, litakuwa la pili baada ya Carabao alilonyakua mwaka jana Kwa kuilaza Newcastle.

Boniface Musotsi
+ posts