Home Michezo Man Utd watoka nyuma na kuilaza Aston Villa Ligi Kuu ya Uingereza

Man Utd watoka nyuma na kuilaza Aston Villa Ligi Kuu ya Uingereza

0

Ilikuwa afueni kwa vigogo wa soka Uingereza Man Utd baada ya kutoka nyuma na kuishinda timu ya Aston Villa magoli 3-2 katika mchuano wa ligi kuu ya Uingereza uliosakatwa katika uwanja wa Old Trafford jana Jumanne. 

Aston Villa ilikuwa imechukua uongozi wa mechi hiyo kwa kutia kimiani magoli 2 hadi kufikia wakati wa mapumziko.

Lakini vijana wake Ten Hag walijituma mchezoni na kusawazisha magoli hayo kupitia kijana matata Garnacho aliyetikisa wavu mara mbili na kufanya mambo kuwa 2-2.

Rasmus Hojlund aliifungia Man Utd bao lake la kwanza kwenye ligi kuu na la ushindi katika mechi hiyo na kufanya mashetani wekundu kupanda hadi nafasi ya 6 kwenye msimamo wa la ligi kuu ya Uingereza baada ya kucheza mechi 19.

Man Utd imekuwa ikiandikisha matokeo duni msimu huu na wengi kutilia shaka ikiwa inaweza kumaliza katika nafasi ya timu nne bora ligini.

 

Website | + posts