Mamia ya Wakenya wangali wamekwama nchini Lebanon kufuatia mashambulizi ya majeshi ya Israel huku ikiripotiwa kuwa zaidi ya watu 45 wamefariki usiku wa kuamkia leo.
Hali ya hofu imetanda miongoni mwa Wakenya walio nchini Lebanon licha ya serikali kusisitiza kuwa wote wako salama.
Imeripotiwa kuwa watu wapatao laki moja wamelazimika kuhama mapema leo kukimbilia usalama wao kufuatia shambulizi jipya kusini mwa Lebanon.
Majeshi ya Israel pia yameripoti kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah kupitia kwa shambulizi la anga.