Home Kimataifa Mamia watoroka mafuriko Delhi

Mamia watoroka mafuriko Delhi

Wakazi 2,500 mjini Delhi karibu na mto, walilazimika kuhamia kambi za kutoa misaada siku ya Jumatano .

0

Mamia ya wakazi wamehamishwa katika mji mkuu wa India,Delhi huku viwango vya maji mtoni Yamuna vikiendelea kupanda.

Kulingana na waziri Arvind Kejriwal,kiwango cha maji katika mto huo kilikuwa cha juu zaidi kuwahishudiwa katika kipindi cha miongo minnne unusu na kuhatarisha maisha .

Viwango vya juu vya mvua vimekuwa vikishuhudiwa tangu mwezi Juni mwaka huu na tayari watu 88 wamefariki eneo la Himachal Pradeh karibu na mji wa Delhi.

Wakazi 2,500 mjini Delhi karibu na mto, walilazimika kuhamia kambi za kutoa misaada siku ya Jumatano .

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here