Home Habari Kuu Mamia waandamana Nairobi kupinga mauaji ya wanawake

Mamia waandamana Nairobi kupinga mauaji ya wanawake

0

Mamia ya wanawake na wanaume wamejitokeza katika barabara za jiji la Nairobi mapema Jumamosi kupinga mauaji ya wanawake wenzao yanayotekelezwa na wanaume.

Wanawake hao wamelalama kuhusu ongezeko la visa vya wanaume kuwatoa uhai wanawake wakitaka haki kwa waliouawa.

Haya yanajiri kufuatia vifo vya Wahu Mwangi na Rita Waeni waliouawa katika vyumba vya kupangisha maarufu kama AirbNb mapema mwaka huu.

Wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe kama vile ‘love does’nt hurt,Stop femicide na women deserve to live wanawake hao walizunguka jijini Nairobi wakiwa wamevalia T shirts nyeupe .

Mbunge wa kaunti ya Nairobi Esther Pasaris alikuwa miongoni mwa waandamanaji hao.

Wanawake hao walitaka haki itendeke kwa familia za wanawake waliouawa kinyama na wanaume.