Home Habari Kuu Mameneja wa kampuni ya Brown Cheese wakamatwa na polisi

Mameneja wa kampuni ya Brown Cheese wakamatwa na polisi

0

Mameneja wa kampuni ya Brown Cheese iliyoko Tigoni, kaunti ya Kiambu wamekamatwa na maafisa wa polisi.

Hii ni kufuatia ufichuzi wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwamba wafanyakazi wa kike walilazimishwa kuvua nguo zao za ndani ili kubaini aliyekuwa na hedhi.

Wasimamizi wa kampuni hiyo wanasemekana kukerwa na sodo iliyotumika na ambayo ilipatikana kwenye jaa la taka ambalo halitumiki kwa sababu hiyo.

Waliokamatwa ni meneja wa kuhakikisha ubora wa bidhaa na meneja wa maswala ya wafanyakazi.

Uchunguzi wa maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Tigoni ulibainisha kwamba sio mara ya kwanza wanawake wa kampuni hiyo wanalazimishwa kuvua nguo.

Seneta mteule Gloria Orwoba ndiye aliyefichua habari hizo leo Alhamisi. Alisema alipigiwa simu na akawasiliana na usimamizi wa kampuni hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here