Home Burudani Mamake Wizkid azikwa

Mamake Wizkid azikwa

0

Mama mzazi wa mwanamuziki Ibrahim Ayodeji Balogun maarufu kama Wizkid alizikwa Ijumaa Oktoba 13, 2023 baada ya ibada katika kanisa la Redeemed Christian Church of God huko Victoria Island, jimboni Lagos nchini Nigeria.

Mama huyo kwa jina Juliana Bolagun aliaga dunia Agosti 18, 2023.

Akizungumza katika hafla ya mazishi, Wizkid ambaye alitiririkwa na machozi alisema kwamba hajawahi kuhisi uchungu kama ambao alihisi alipompoteza mama mzazi.

“Ninajua uchungu huu hauwezi kuondoka kwa hivyo sitaomba kwamba uniondokee lakini ninajua Mungu atatufariji kama familia ili tuweze kuendelea na maisha.” alisema mwimbaji huyo.

Mama Juliana ameacha watoto wanne ambao ni Yetunde, Omolara, Olubusayo na Ayodeji (Wizkid) na wajukuu 9.