Home Burudani Mamake Kanumba asema huwa hatazami filamu za marehemu mwanawe

Mamake Kanumba asema huwa hatazami filamu za marehemu mwanawe

0
kra

Mama mzazi wa msanii Stephen Kanumba kwa jina Flora Mutegoa amesema kwamba huwa anapata ugumu sana kutizama filamu alizoigiza marehemu mwanawe.

Akizungumza alipowasili jana Jumamosi Septemba 7, 2024 katika uwanja wa Leaders jijini Dar es Salaam kwa ajili ya tamasha ya “Faraja ya Tasnia” Flora alisema kila akijaribu kuangalia filamu hizo huwa anajawa majonzi.

kra

Flora ambaye aliingilia uigizaji baada ya Kanumba kuaga dunia alikuwa akijibu swali la mwanahabari aliyetaka kujua filamu ambayo anapenda zaidi kati ya zote alizoigiza Kanumba.

“Kwanza tangu ameondoka duniani siangalii filamu zake. Nimejitahidi sana ila nashindwa. Movie zake zote nazipenda ila huwa siziangalii.” alisema Flora.

Alishukuru waandalizi wa hafla hiyo akisema kwamba hata ingawa wapendwa wao hawako duniani kimwili wako kiroho na ni vywema kuwakumbuka.

Hafla hiyo iliandaliwa na mwigizaji Steve Nyerere na wenzake na ilihudhuriwa na viongozi wa sekta ya burudani nchini Tanzania na hata wamiliki wa vyombo vya habari.

Eneo la tukio lilikuwa limepambwa na picha za wasanii waliotangulia mbele za haki wakiwemo wanamuziki, waigizaji, wachekeshaji na hata “promoters” kama Ruge Mutahaba”.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Kedmon Mapana alihudhuria hafla hiyo akisema kwamba hangekosa kwa sababu yeye ni mmoja wa waliopatiwa jukumu la kulea na kuwaelekeza wasanii nchini Tanzania.

Website | + posts