Home Burudani Mamake Jay Z afunga ndoa na mpenzi wake

Mamake Jay Z afunga ndoa na mpenzi wake

0

Mama mzazi wa mwanamuziki Jay Z, Gloria Carter, alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Roxanne Wilshire Jumapili usiku jijini New York nchini Marekani.

Beyoncé, Kelly Rowland, Tina Knowles-Lawson, Tyler Perr na Robin Roberts ni kati ya watu tajika ambao walihudhuria harusi hiyo huko Tribeca.

Jay-Z ndiye alifahamisha umma kuhusu mamake kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwenzake kupitia kwa kibao “Smile” ambacho kipo kwenye albamu yake ya mwaka 2017 inayofahamika kama “4:44”.

Kwenye wimbo huo anaimba, “Mama alijaliwa watoto wanne lakini ni msagaji, alijisingizia na kujificha muda mrefu ili kuepuka kulaumiwa na umma. Nililia machozi ya furaha ulipoingia kwenye mapenzi, sijali kama ni mume au mke nataka tu kukuona ukitabasamu.”

Jay alielezea kwenye mahojiano kwamba mamake alimjuza hali ya uhusiano wake wa kimapenzi wakati alikuwa akiandaa albamu hiyo ya 4:44 na kesho yake akawa ameandika wimbo kumhusu.

Katika wimbo huo kuna shairi ambalo limeandikwa na Gloria mwenyewe na anasema aliliandika akiwa kwenye ndege kuelekea Los Angeles kumuona mwanawe.

Gloria aliona anastahili kumsaidia Jay Z kumaliza kuandika wimbo huo na Jay alimrekodi akisoma shairi hilo kwenye mawasiliano ya simu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here