Home Kaunti Mama awateketeza wanawe kaunti ya Kajiado

Mama awateketeza wanawe kaunti ya Kajiado

0

Mwanamke mmoja mwenye umri wa makamu ameteketeza nyumba yake na kusababisha vifo vya wanawe wawili wa umri wa miaka miwili na kumi mtawalia.

Kisa hicho kilichotokea katika mtaa wa Saina mjini Kajiado kilitokana na mzozo wa nyumbani.

Inasemekana kuwa mama huyo alitekeleza uovu huo baada ya kugundua kuwa mumewe alikuwa ameoa mke wa pili.

Anadaiwa kuwafungia ndani ya nyumba watoto hao na kufungua mtungi wa gesi kabla ya kuwasha moto.

Mwanamke huyo aliokolewa na majirani na kupelekwa katika hospitali ya Kajiado anakouguza majeraha.

Hata hivyo, watoto hao wawili waliteketea kiasi cha kutoweza kutambulika.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kajiado ya Kati Daudi Loronyokwe, alisema mili ya watoto hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya matibabu maalum ya Kajiado huku mama akiendelea kupokea matibabu katika hospitali hiyo.

Kulingana na majirani, mwanamke huyo na mumewe wamekuwa wakizozana katika miezi ya hivi karibuni na  hata walizozana kabla ya tukio hilo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here