Home Michezo Malkia Strikers watwaa ubingwa wa Afrika

Malkia Strikers watwaa ubingwa wa Afrika

0

Timu ya taifa ya Voliboli ya Wanawake maarufu kama Malkia Strikers ndio mabingwa wa Afrika baada ya kuwachakaza Misri seti tatu kwa bila kwenye fainali iliyosakatwa jana Alhamisi mjini Yaounde nchini Cameroon.

Kenya walishinda mechi hiyo kwa seti 25-22, 25-20 na 25-16.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Kenya tangu mwaka 2015 ikiwa taji ya 10 kwa jumla.

Wenyeji Cameroon walinyanyakua nishani ya shaba baada ya kuishinda Rwanda seti 3-1.

Website | + posts