Home Michezo Malkia Strikers watinga fainali ya Kombe la Afrika na kufuzu kwa Olimpiki...

Malkia Strikers watinga fainali ya Kombe la Afrika na kufuzu kwa Olimpiki mwaka 2024

0

Timu ya taifa ya voliboli ya wanawawake almaarufu Malkia Strikers imejikatia tiketi ya kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka ujao jijini Paris nchini Ufaransa baada ya kufuzu kwa fainali ya mashindano ya kuwania Kombe la Afrika .

Kenya ilitoka nyuma na kuwazabua wenyeji Cameroon seti 3-1 katika nusu fainali ya Jumatano kwa seti za  25-25, 25-14, 25-11 na 25-18.

Malkia watakumbana na miamba Misri katika fainali siku ya Alhamisi usiku,baada ya Misri kuwalemea  Rwanda seti tatu kwa nunge.

Timu zote mbili pia zimefuzu kwa mashindano ya dunia.