Home Michezo Malkia Strikers waishinda Rwanda mechi ya ufunguzi mashindano ya Voliboli Afrika

Malkia Strikers waishinda Rwanda mechi ya ufunguzi mashindano ya Voliboli Afrika

0

Timu ya taifa ya Kenya ya Voliboli kwa wanawake Malkia Strikers imeanza harakati za kuwania kombe la Afrika  katika makala ya 21 kwa ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Rwanda Jumatano nchini Cameroon.

Malkia wameshinda kwa seti za 25-16,25-20 na 25-27 .

Kenya chini ya ukufunzi wa kocha Paul Bitok pia itamenyana na Morocco,Uganda, Burkina Faso na Lesotho katika kundi B .

Kundi A linasheheni Mali,Nigeria,Misri na Algeria,Burundi na wenyeji Cameroon.

Mashindano hayo yatakamilika tarehe 26 mwezi huu mjini Yaounde Cameroon.

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here