Timu ya taifa ya voliboli ya wanawake imesajili ushindi wa tatu mtalia katika mashindano ya kuwania Kombe la Afrika yanayoendelea mjini Yaounde nchini Cameroon.
Kenya, almaarufu Malkia Strikers, wameibwaga Uganda seti 3 kwa bila za 25-15, 25-16 na 25-14 katika mchuano uliopigwa uwanjani Mfandena.
Kocha mkuu wa Kenya Luizomar de Moura alifanya mabadiliko matatu kwenye pambano hilo akiwajumuisha Rose Magoi kutwaa nafasi ya Emmaculate Nekesa na Loice Simiyu Sharon Chepchumba huku Belinda Barasa akipumzishwa na nafasi yake kushikiliwa na Edith Wisah.
Kenya imezoa alama 9 baada ya kusajili ushindi dhidi ya Rwanda, Burkina Faso na Uganda.