Ndoto ya Kenya kupata ushindi wa kwanza katika michezo ya Olimpiki haijatimia, baada ya timu ya taifa ya Vliboli ya wanawake kuambulia kichapo cha seti 3-0 dhidi ya miamba wa dunia Brazil.
Mchuano huo wa ufunguzi wa olimpiki kundini B uliochezwa jijini Paris, huku vipusa wa Samba, wakishinda seti ya kwanza 25-14 na kuimarisha mchezo wao katika seti 2 za mwisho 25-13 na 25-12.
Pambano hilo lilichukua dakika 56 pekee kukamilika huku wakijiandaa kwa mchi ya pili kesho kutwa dhidi ya Poland na kisha kukamilisha ratiba Agosti 3 dhidi ya Japan.
Malkia Strikers wanashiriki Olimpiki kwa mara ya nne ,mwaka 2000,2004,2020 na 2024.