Home Burudani Malia Obama ahudhuria tamasha la filamu ya Deauville, Ufaransa

Malia Obama ahudhuria tamasha la filamu ya Deauville, Ufaransa

0
kra

Malia Ann Obama binti wa kwanza wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama, alihudhuria awamu ya 50 ya tamasha la filamu ya Deauville almaarufu “Deauville American Film Festival”  nchini Ufaransa hivi maajuzi, suala lililochangamsha wapenzi wa tamasha hilo.

Malia ambaye aliingilia kazi ya uaandaaji filamu mwaka 2022 alihudhuria hafla hiyo kutokana na filamu yake fupi kwa jina “The Heart”.

kra

Akizungumza na wanahabari, binti huyo alielezea kwamba filamu yake inahusu upweke, kupoteza uwapendao na upatanisho na watu ambao huenda wakasaidia kuondoa upweke.

Punde baada ya kumaliza masomo katika Chuo Kikuu cha Harvard, Malia aliingilia tasnia ya filamu na kazi hiyo yake ilizinduliwa rasmi kwenye tamasha la filamu ya Sundance huko Park City katika jimbo la Utah, Januari 18, 2024.

Akiwa nchini Ufaransa, Malia alisema kwamba anafurahia kuhudhuria hafla kama hiyo, hata ingawa alikuwa na woga kidogo kwani ndio mara ya kwanza.

Vazi lake ambalo lilikuwa limeundwa kutokana na kile kilichoonekana kuwa vipande vya shati alisema liliundwa na msanifu mavazi Vivian Westwood ambaye alimrejelea kama “Malkia”.

“Sijui mengi kuhusu mitindo ya mavazi lakini nafurahia kuvaa hili,” alisema Malia alipokuwa akihojiwa na wanahabari kwenye “red carpet” ya Vanity Fair.

Website | + posts