Jeshi la Kenya limetangaza uteuzi wa jumla ya makurutu 1,606 waliofaulu katika uteuzi wa kitaifa ulioandaliwa baina ya mwishoni mwa Agosti na mwanzoni mwa mwezi huu.
Kati ya idadi hiyo, makurutu 347 wanajiunga na jeshi kama wataalamu huku wengine 1,259 wakijiunga kama makurutu wa kawaida.
Walioshiriki zoezi hilo wanaweza kubaini uteuzi kwa kutembelea tovuti ya mod.go.ke.
Makurutu wa kawaida wa kiume na kike wanatikiwa kuripoti Embakasi Garrison Septemba 27 kuanzia saa mbili asubuhi kwa usaili.
Kwa upande mwingine, makurutu wataalam wanatikiwa kuhudhuria usaili katika chuo cha KMA Lanet kaunti ya Nakuru.
Usaili huo utafuatwa na mafunzo ya miezi sita kwa makurutu kabla ya kufuzu na kutumwa katika vituo tofauti.
Wale ambao hawakufaulu watarejeshewa nauli waliyotumia wakati wa kuhudhuria uteuzi.