Home Kaunti Makundi ya kimaendeleo kupewa ruzuku kujiendeleza kiuchumi Kakamega

Makundi ya kimaendeleo kupewa ruzuku kujiendeleza kiuchumi Kakamega

0
kra

Serikali ya kaunti ya Kakamega imeahidi kuyapatia ruzuku makundi ya kimaendeleo katika kaunti hiyo.

Ahadi hiyo imetolewa na Gavana wa kaunti hiyo Fernandes Barasa.

kra

Ili kudhihirisha ahadi yake, Barasa, wakati akizungumza katika uwanja wa Musoli katika eneo la Ikolomani, alitoa ruzuku za thamani ya shilingi  50,000 kwa makundi 900 ya vijana na wanawake.

Alisema makundi 15 katika kila wadi yamepokea ruzuku na kuahidi kusaidia makundi mengine ili kujiendeleza.

Alitoa changamoto kwa makundi yaliyopokea ruzuku kujikwamua kiuchumi.  

Kadhalika, Gavana huyo alimpongeza Rais William Ruto kwa kumteua mtangulizi wake Wycliffe Oparanya kuwa Waziri wa Ustawi wa Vyama vya Ushirika na Biashara Ndogo Ndogo huku akiwataka wabunge kuhakikisha wanawahakiki kwa kina walioteuliwa.